Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa badala ya kulipigia kelele katika
mitandao ya kijamii suala la mabadiliko ya Katiba, watanzania kwanza wachape
kazi na Katiba itafuata kwa wakati wake.
Akizungumza wakati wa kuchangia
kwenye kongamano la kujadili hali ya uchumi na siasa katika kipindi cha miaka
mitatu ya utawala wake, Rais Magufuli amesema kuwa hategemei kutenga fedha kwa
sasa kwa ajili ya kurejesha mchakato wa Katiba mpya.
"Nafahamu hamu ya
watanzania kuwa na katiba mpya, sasa tunafanyaje!? Tunaendelea na hii rasimu
pendekezwa au tunaenda kwenye ile ya kwanza iliyofanywa na Jaji Warioba!? Sasa
badala ya kuanza kujibizana na haya ngoja tuchape kazi", amesema
Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amebainisha kuwa
anakutana na changamoto pindi anapofanya uteuzi mbalimbali hasa kwa wanawake
ikiwemo madai anayopelekewa ambayo hayana ukweli na kuahidi kuendelea kuwapa
nafasi kwenye uongozi wake
Kwa mujibu wa Rais Magufuli wakati
akifanya uteuzi wa wanawake amekuwa akituhumiwa kuteua watu ambao ana mahusiano
nao mbali na mahusiano ya kikazi.
“Nimeteua kina mama wengi, na
sasa hivi kila unayemteua kina mama ni hawara yako, na nitaendelea kuwateua tu,
kuna wakati wanaofanya hivi ni kina mama wenyewe, sijui wanataka niteue wanaume
tu, mimi nitaendelea kuwateua", amesema Rais Magufuli.
Magufuli aibua suala la Katiba mpya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment