Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa amezuiwa kumuona kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe
anayeshikiliwa na polisi tangu jana Oktoba 31, 2018.
Msaidizi wa waziri mkuu huyo wa
zamani, Aboubakary Liongo amesema kuwa leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018
saa 9 Alasiri Lowassa alikwenda kumuona Zitto kutaka kujua hatima yake, kwani
wako pamoja naye kuhakikisha haki inatendeka, lakini akaelezwa kuwa muda wa
kumuona umeshapita.
Baada ya kufika kituoni hapo,
msaidizi wa Lowassa alikwenda kuomba kibali cha kumuona Zitto lakini alielezwa
kuwa muda umekwisha, ambapo Lowassa amenukuliwa akisema, “Huyu ni
kiongozi mwenzetu huku upinzani lazima tushikamane kukabiliana na lolote lililo
mbele yetu, tunahitaji kuwa kitu kimoja kuliko wakati mwingine wowote".
Zitto yupo kituo cha polisi
Mburahati ambako alipelekwa jana baada ya kutolewa kituo cha kati Polisi makau
makuu akitokea kituo cha Osterbay alikohojiwa kwa zaidi ya saa 3 baada ya
kukamatwa akiwa nyumbani kwake jijini Dar es salaam.
Lowassa azuiwa Polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment