Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
imeelezwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameshindwa kufika
mahakamani kwa kuwa amepelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu, ambapo
inadaiwa Mbowe anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na shinikizo la damu.
Kauli hiyo imetolewa mahakamani leo
Novemba 1 na mdhamini wa Mbowe, Grayson Celestine aliyedai kuwa amepewa taarifa
za ugonjwa wa Mbowe na mke wa mwanasiasa huyo.
"Kwa mujibu wa maelezo ya
mkewe, Mbowe anasumbuliwa na matatizo ya moyo pamoja na shinikizo la damu na
familia imeamua kumsafirisha afrika kusini kwa dharura lakini mimi sijaonana
naye" amesema Celestine.
Aidha Celestine alimueleza Hakimu
Mashauri kuwa “mshtakiwa Freeman Mbowe akirejea atawasilisha nyaraka za safari
na matibabu, kwamba anaendelea kufanya mawasiliano ili azitume nyaraka kwa njia
ya mtandao.”
Kufuatia maelezo hayo, wakili wa
Faraja Nchimbi aliomba kutolewa kwa amri ya kumkamata Mbowe ili ajieleze sababu
za kutofika mahakamani.
“Sisi upande wa mashtaka hiyo
tunaona ni mwendelezo wa dharau ya mshtakiwa Mbowe kwa mahakama kwa kuwa
alishapewa onyo, Mbowe ameamua kwa utashi wake kukiuka amri ya mahakama”,
amesema Faraja Nchimbi.
Kiongozi huyo wa CHADEMA na viongozi
wengine wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuratibu na kufanya
maandamano yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi Chuo cha Taifa
Usafirishaji NIT, Akwilina Akwilini.
Sababu ya Freeman Mbowe kukimbilia Afrika Kusini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment