SERIKALI
imemaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya wakulima wa chai wa wilaya
za Lushoto na Korogwe na kampuni ya Mponde Tea Estate uliosababisha kufungwa
kwa kiwanda cha chai cha Mponde baada ya kuagiza kiwanda hicho kianze kazi.
“Waziri
Mwijage na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilomo Prof. Siza Tumbo hakikisheni kazi
ya kukagua kiwanda na mitambo inafanyika haraka na kubaini mitambo ipi ni
mizima na ipi ina hitilafu ili ukarabati ufanyike na kiwanda kianze kazi mara
moja.”
Uamuzi
huo wa Serikali umetangazwa leo (Alhamisi, Novemba 1, 2018) na Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye kijiji cha Kweminyasa kata ya Mponde, wilayani Lushoto baada
ya kutembelea kiwanda hicho .
Waziri
Mkuu amesema mwaka 1999 Serikali iliamua kuwapa wakulima wa chai na kiwanda
hicho kwa ajili kuwawezesha kuwa na sehemu ya kuchakata chai yao
lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi. Imeamua kukirudisha Serikali
baada ya kuwepo migogoro iliyoathiri uzalishaji kiwandani hapo.
Kuhusu
suala la madeni ya watumishi, ameagiza watafutwe na madai yaorodheshwe kwa
ajili ya malipo, amewahakikisha wananchi hao kuwa suala la ajira ambazo
zilipotea baada ya kiwanda kufungwa zitarudi kwa sababu Serikali inataka kuona
kiwanda kikifanya kazi.
“Serikali
imeamua kukichukua kiwanda hiki ambacho awali ilikikabidhi wakulima wa chai na
kwamba itahakikisha lengo lake la kuboresh kilimo linafanikiwa
na wakulima wanaendelea kulima zao la chai. Hatutaki kusikia masuala
ya Utega wala Mponde hapa si mahali pake.”
Amesema
wakulima hao walikosea kwa kuunda Umoja wa Wakulima wa Chai (UTEGA) ambapo
katika kusajili badala ya kuanzisha ushirika wao walisajili NGO ambayo ilikuwa
na wanachama wake, huku kiwanda kikiwa kimeanzishwa kwa ajili ya wakulima wote,
jambo ambalo lilisababisha mgogoro baina ya wakulima na viongozi wa UTEGA.
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa wakati mgogoro huo ukiendelea kati ya UTEGA na wakulima wa
chai wasiokuwa wanachama wa NGO hiyo, uliibuka mgogoro mwingine baina ya
wakulima wote pamoja na muwekezaji ambaye ni kampuni ya Mponde Tea Estate baada
ya kukabidhiwa kiwanda hicho na uongozi wa UTEGA bila ya wao
kushirikishwa.
Amewasisitiza
wakulima wafufue mashamba yao kiwanda ni
cha Serikali hivyo watakuwa wamepata sehemu ya uhakikika
ya kupeleka chai ambayo itachakatwa. Pia ameagiza Mrajisi wa Ushirika aende kwa
wakulima na kutambua idadi yao pamoja na
kujua ukubwa
wa mashamba yao.
Amesema
baada ya kubaini idadi ya wakulima na ukubwa wa mashamba yao awasaidie katika
kuunda vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kisha kuunda ushirikia wao ambao
watautumia katika kusimamia zao lao la chai na kuhakikisha mkulima ananufaika.
Waziri
Mkuu amesema zao la chai ni miongoni mwa mazao makuu sita ya kimkakati, mengine
ni korosho, kahawa, tumbaku, pamba na chikichi, hivyo amewataka wafufue
mashamba yao na waendelee kuiamini Serikali yao ambayo imejidhatiti
kuwahudumia.
Awali,Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makam wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba alisma
Mgogoro huo wa kiwanda cha Mponde ulianza tangu mwaka 1999 na ilipofika mwezi
Mei 2013, wananchi walimlalamikia kwa kushindwa kutatua tatizo hilo.
Makamba
ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli aliwaomba wananchi hao waendelee kuwa na subira
wakati suala lao likiwa linaendelea kushughuliwa na Serikali. “Mgogoro huo
umesababaisha kudhorota kwa uchumi kwa sababu wananchi wengi waliacha kulima
chai baada ya kiwanda hicho kufungwa miaka mitano iliyopita.”
HIvyo
Makamba ameiomba Serikali iwasaidie wakulima wa zao la chai kuwapa miche mipya
pamoja na pembe jeo kwa ajili ya kufufua zao hilo na kukiwezesha kiwanda cha
chai MPonde kupata malighafi kama ilivyokuwa hapo awali.
Kwa
upande wake, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
alisema kuwa tayari amekuja na wataalam kwa ajili ya kukagua mashine
zote zilizopo kiwandani hapo ili mchakato wa kukiwasha uanze mara
moja.
Mwijage
alisema “mimi kama Waziri mwenye dhamana ya viwanda nawaambia wananchi muondoe
wasiwasi tayari kiwanda kimeshafunguliwa maana sitaondoka hapa Bumbuli mpaka
kieleweke.”
Waziri Majaliwa amaliza Mgogoro wa Kiwanda cha Mpombe Lushoto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment