Bunge la EALA lapitisha Muswada wa Sheria Sarafu ya Pamoja


Bunge la Afrika mashairiki (EALA)jana limepitisha Muswada wa sheria ya Takwimu ambapo muswada huo ni muhimu sana wakati jumuiya hiyo inaelekea kwenye sarafu ya pamoja.

Akichangia katika bunge hilo Mbunge wa Afrika Mhandishi Mohammed Habibu Mnyaa amesema kuwa muswada huo umekuwa umerudiwa rudiwa  sana na hivyo kuchukuwa muda mrefu hadi kupitiswa kwake.

Amesema kuwa kuchukuwa muda mrefu ilikuwa ni kutaka baadhi ya tafsiri zirekebishwe hususani zilizokuwa zinailenga Nchi ya Tanzania ikiwemo ya wakuu wa bodi za takwimu kuwa wajumbe katika kamati.

Jambo hilo lilipelekea kupigana hadi kuhakikisha kuwa muswada huo unapitisha wajumbe huru kuingia katika kamati na wakuu hao kuwa huru kama wajumbe ili kuepusha nchi kuleta takwimu zenye maslahi na taifa lao.

“Muswada huu utasaidia sana wakati nchi za jumuiya zikielekea kwenye sarafu moja ambapo nchi wanachama zitaleta wajumbe huru ambao wataleta takwimu sahihi zitakazosaidia nchi yetu na jumuiya kulinda maslahi”alisema Mhandisi Mnyaa.

Amsema kuwa kila wakati muswada huo ulikuwa unarudiwa kwa sababu tulitaka baadhi ya tafsiri zirekebishwe hususani zilizokuwa zinailenga nchi ya Tanzania hivyo kupitishwa italeta faida kwa jumiya yetu.

Kupitisha muswada huo na kupitisha kufingu kinachopinga wakuu wa takwimu wan chi wanachama kuwasilisha muswada wa takwimu kwa kamati itakuwa ni kuleta takwimu zinazoleta unafuu kwa nchi zao.
Bunge la EALA lapitisha Muswada wa Sheria Sarafu ya Pamoja Bunge la EALA lapitisha Muswada wa Sheria Sarafu ya Pamoja Reviewed by KUSAGANEWS on November 01, 2018 Rating: 5

No comments: