Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul
Makonda amepinga moja ya hoja zilizotolewa na wahudhuriaji wa kongamano hilo,
ikiwemo hoja iliyosema kwamba alidai asilimia kubwa ya wateule wa Rais wamekuwa
wakitumia vibaya mamlaka yao.
Akichangia kwenye kongamano hilo
Makonda amesema kuwa idadi kubwa ya watu wanaolalamika matumizi mabaya ya
wateule hao wa Rais walikuwa wanufaika wa mfumo mbovu.
“Rais hajamtuma RC na DC kutumia
mamlaka vibaya, kupima utendaji wa Rais Magufuli ni kama kutoa treni barabarani
kuirudisha kwenye reli, kwa hiyo lazima kuna vyuma lazima vitalalamika,
niwaombe tusichukulie matukio machache yanatokea kuwa ni maagizo ya Rais”,
amesema Paul Makonda.
Awali Mbunge mteule wa Jimbo la
Ukonga jijini Dar es salaam, Mwita Waitara amemshauri Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuangalia upya namna ya kuzalisha
ajira kwa vijana ili kupunguza vilio vya ajira.
Akichangia kwenye kongamano la
kujadili hali ya uchumi na siasa katika kipindi cha miaka 3 cha serikali ya
awamu tano, Waitara amesema suala la ajira kwa wananchi wa Tanzania lipewe
kipaumbele.
“Nikushauri mheshimiwa Rais
kuna shida ya ajira Tanzania awaombe wasaidizi wake, wazalishe ajira nchini
hasa kwa vijana, vijana wengi nchini na vijana wanatumika kisiasa naomba ajira
itafutwe ili waweze kuishi”, amesema.
Makonda ajibu kuhusu matumizi mabaya ya mamlaka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment