WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela orodha
ya matrafiki wanaodaiwa kuwaomba rushwa madereva wa noah wilayani Lushoto.
Majina
ya trafiki hao wanadaiwa kuomba rushwa kwa madereva wa noah wanaofanya kazi ya
kusafirisha abiria ndani ya wilaya hiyo yaliwasilishwa kwa Waziri Mkuu kupitia
mabango.
Waziri
Mkuu alimkabidhi majina hayo jana jioni (Jumatano, Oktoba 31, 2018) baada ya
kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Sabasaba, Lushoto mjini.
Baada ya
kumkabidhi majina hayo alimuagiza afanye uchunguzi wa tuhuma za rushwa
zinazowakabili askari hao na kisha awasilishe taarifa kwake leo Alhamisi
Novemba 1, 2018.
Mbali ya
wananchi kuwasilisha malalamiko hayo, Pia mbunge wa Lushoto, Shaaban Shekilindi
alimuomba Waziri Mkuu awasaidie kutatua kero hiyo inayowakabili wananchi.
Awali, Waziri
Mkuu alizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Lushoto katika ukumbi
wa chuo cha Mahakama Lushoto ambapo aliwasisitiza wafanye kazi kwa bidii.
Alisema
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haina msamaha
na mtumishi wa umma asiyetaka kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi.
Alisema
watumishi wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa kufuata maadili ya utumishi ili
waweze kutimiza lengo la Serikali la kuwahudumia wananchi kwa kutumia taaluma
zao.
Waziri
Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Tanga
alisema Serikali haina msamaha na mtumishi asietaka kubadilika na kufanya kazi.
Pia, Waziri
Mkuu aliwataka watumishi wa umma wahakikishe fedha zinazotolewa na Serikali kwa
ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo zinatumika kama
ilivyokusudiwa.
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwataka Wakuu wa Idara kutumia kitabu cha ilani ya uchaguzi cha
CCM cha mwaka 2015/2020 kwa sababu kina maelekezo wanayopaswa kuyatekeleza.
“Kitabu
kile kina maelezo ya msingi yaliyotolewa na Rais. Dkt. Magufuli ambayo
yanatakiwa yapewe kipaumbele cha utekelezwaji, wakuu wa Idara ni muhimu musome
na kutekeleza.”
Waziri
Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka wakuu wa wilaya wahakikishe wanasimamia
utekelezwaji wa maelekezo yote yaliyoainishwa kwenye kitabu cha Ilani katika
maeneo yao.
Kuhusu
changamoto ya upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali nchini, Waziri Mkuu alisema
Serikali inatambua na kwamba suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu alizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba na kuwapongeza wakazi hao kwa kutunza
misitu.
Alisema maeneo
mengi nchini wananchi wamekata miti na kusababisha kukauka kwa vyanzo vya maji,
ambapo ni tofauti na wilaya ya Lushoto ambayo bado ina misitu minene.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wote wa vijiji na kata waainishe
sehemu zote zenye misitu na vyanzo vya maji katika maeneo yao na
wahakikishe wanayalinda.
Alisema
mtu yeyote atakayebainika kuharibu mazingira hayo iwe kwa kuchoma au kukata
miti achukulie hatua kali. “Ni marufuku mtu yeyote kukata miti bila kibali cha
Serikali.”
Nae,
Mbunge wa Lushoto Shekilindi
alimuomba Waziri Mkuu awasaidie katika kuwatatulia changamoto mbalimbali
zinazowakabili wananchi wa katika jimbo hilo ikiwemo ya afya.
Mbunge
alisema kwa sasa hospitali ya wilaya hiyo inakabiliwa na ukosefu wa mashine ya
x
rey,
hivyo kusababisha wananchi kusafiri hadi Korogwe au Tanga kufuata huduama hiyo.
Waziri
Mkuu alisema tayari ameshamuagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kupeleka mashine ya x-rey katika hospitali hiyo.
TRAFIKI Waomba Rushwa Washtakiwa kwa Waziri Mkuu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 01, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment