Mkuu wa Mkoa wa
Tabora, Agrey Mwanri amesema wakuu wake wa Wilaya wameanzisha utaratibu maalum
wa kuwakagua wageni wanaoingia mkoani humo kwa lengo la kutokomeza biashara
haramu ikiwemo ya ukahaba, na madawa ya kulevya.
Katika maelezo yake, aligusia suala la biashara ya ukahaba mkoani humo ambapo amesema kuwa wengi miongoni mwa watu hao wamekuwa wakitokea mikoa mingine hasa Dar es salmaa na kuingia mkoani humo.
“Ukienda kwenye nyumba za wageni za Tabora, utashangaa kumuona mtu anatakata tu lakini hujui biashara anayofanya, nimewagiza wakuu wangu wa wilaya wakipita watu ambao hawajulikani wakaguliwe kazi gani wanafanya", amesema Mwanri.
Kuhusiana na suala la elimu Agrey Mwanri amesema mpango wake ni kuhakikisha kila nyumba ya mkazi wa Tabora inafanikiwa kutoa muhitimu wa elimu ya Chuo Kikuu.
Mwanri amesema “ukitaka wananchi wako wawe na vifaa waelemishe watu wako, usiwadharau, tunalofanya na mpango tulionao ni kutoa wahitimu wa chuo kikuu katika kila nyumba ya mkazi wa Tabora, hata bibi kizee mwenye miaka 80 atapata degree (Shahada ya kwanza) lakini miaka 30 ijayo hatakuwepo ndio maana tunawekeza kwa watoto.”
Mwanri amjibu Makonda,aja na lake suala la ushoga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment