WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuboresha
huduma za afya kwenye maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya halmashauri ya
wilaya ya Lushoto.
Amesema
lengo ni kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya chenye uwezo wa kutoa
huduma mbalimbali muhimu zikiwemo za maabara, upasuaji na mama na mtoto.
Ametoa
kauli hiyo leo wakati akizungumza na wakananchi katika kata ya Malindi, baada
ya kutembelea jengo la soko mbogamboga la Malindi.
Waziri
Mkuu amesema Serikali imejipanga vizuri katika sekta ya afya baada ya bajeti ya
kununulia dawa kuongezeka kutoka sh. bilioni 31 kwa mwaka na kufikia bilioni
269.
“Hatutaki
tena kusikia mgonjwa anaenda hospitali na kukosa dawa biashara hiyo
tumeimaliza, Rais Dkt. John Magufuli ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi
wa dawa.”
Amesema
katika wilaya ya Lushoto Serikali imetenga sh. bilioni 1.4 kwa ajili ujenzi na
ukarabati wa majengo ya vituo vya afya vya kata za Kangagai. Mnazi na Mlola.
“Halmashauri
wekeni mpango thabiti wa kujenga wodi mbili kati yake moja ya wanaume na
nyingine ya wanawake, lengo la Serikali ni kuboresha huduma za afya kwa
wananchi.”
Aizungumzia
kuhusu mradi wa ujenzi wa soko, Waziri Mkuu amesema mradi huo ni sehemu ya
huduma zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha huduma za jamii nchini.
Waziri
Mkuu ametaja huduma nyingine zinazotolewa na Serikali kwa wananchi ni za afya,
elimu, maji, uchumi na ujenzi na uboreshwaji miundombinu mbalimbali ikiwemo ya
barabara.
Hivyo,
amewataka wananchi watumie vizuri soko hilo ambalo linatoa fursa
kwao kufanya biashara katika eneo zuri na kuwawezesha kuuza bidhaa zao zikiwa
katika ubora.
Pia
amewashauri wakulima hao wajiunge katika vikundi na kuanzisha ushirika wao ili
waweze kusaidiwa na Serikali katika kupata mikopo kwa ajili ya kuzalisha kwa
ubora zaidi.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto, Bibi Ikupa
Mwasyoge amesema kukamilika kwa soko hilo kutainufaisha halmashauri na
wananchi.
Bibi.
Ikupa amesema ujenzi wa jengo hilo la soko la ghorofa mbili lililojengwa kwa
awamu mbili ulianza mwaka 2011 na umekamilika Septemba 2018, umegharimu sh.
bilioni 1.1.
Amesema
halmashauri itanufaika kwa kupata ushuru na wananchi ambao wengi wao ni
wakulima wa mboga na matunda watakuwa na sehemu ya uhakika wa kufanyia
biashara.
“Wakulima
35,000 wa kata ya Malindi na kata jirani za Lukozi, Manolo na Shume
wanaozalisha wastani wa tani 5,900 za mboga na matunda kwa mwaka watanufaika.”
Naye,
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
amesema Serikali imefanya kazi kubwa katika kuboresha huduma za afya nchini.
Amesema
bajeti ya dawa katika halmashauri hiyo imeongezeka kutoka sh milioni 183 za
dawa zilizokuwa zinatolewa awani na sasa imefikia sh milioni 565.
Mbunge
wa jimbo la Mlalo, Bw. Rashid Shangazi ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali
kwa kuwasaidia wananchi wa halmashauri kuongeza thamani ya mazao yao kabla ya
kuuza.
Awali,Waziri
Mkuu alizindua jengo la utawala la Halmashauri ya wilaya ya Lushoto
lililogharimu sh. bilioni 4.3. Kukamilika kwa jengo hilo kutaboresha huduma kwa
wananchi.
Waziri Mkuu aikumbuka Wilaya ya Lushoto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment