Takribani watu 9 wamejeruhiwa
kufuatia ajali ya treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRC) iliyotokea katika
eneo la Karakata Ilala jijini Dar es salaam baada ya treni hiyo ya abiria
baadhi ya mabehewa yake kuacha njia na kudodondoka.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dar es
salaam Sophia Mjema akipokea maelezo juu ajali ya \treni iliyotokea asubuhi ya
leo eneo la Kalakata.
Taarifa ya ajali hiyo ilianza
kusambaa kupitia mitandao ya kijamii ambapo ilielezwa treni hiyo ilikuwa
ikitokea Pugu, kuelekea makano makuu yaliyooko Posta kwa ajiili ya kuendelea na
safari zake za kila siku za kusafirisha abiria.
Akizungumza
Kamanda wa Polisi wa Reli Tanzania David Mnyambuga amesema mpaka sasa chanzo
cha ajali hiyo bado hakijajulikana na kudai jeshi hilo linaendelea kuchunguza.
“Leo saa 12 .45 asubuhi treni
hiyo ilipofika maeneo ya karakata Ilala, mabehewa mawili yalidondoka na mengine
matatu yalipotea njia iliacha wataalamu wa reli wanaendelea na uchunguzi”,
amesema Mnyambuga David.
Wakati huohuo Kupitia Mkuu wa Wilaya
ya Ilala Sopghia Mjema alifika eneo la ajali na kuwatembelea baadhi ya majeruhi
wa ajli hiyo ambapo amesema "nimefika Hospitali ya Amana kuwapa pole
majeruhi wa ajali ya Treni, tuendelee kuwaombea kwa mwenyezi Mungu wapate
afueni kwa haraka,hakika wapo katika mikono salama".
Treni hiyo imejibebea umaarufu kama
“treni ya Mwakyembe” kufuatia baadhi ya mabehewa kununuliwa wakati Dkt Harrison
Mwakyemba akiwa Waziri wa uchukuzi, na kuliongoza shirika hilo la reli Tanzania
(TRL) ambalo nalo kwa sasa limebadilika na kuwa Kampuni ya reli ya Tanzania
TRC.
Mwanzoni mwa 2015 aliyekuwa Rais wa
awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza kumuhamisha Dk Mwakyembe
wizara ya Afrika Mashariki kufuatia mabadiliko ya madogo ya baraza la mawaziri.
Chanzo cha ajali , treni ya Mwakyembe leo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment