Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
amewataka waumini na viongozi mbalimbali wa dini nchini kutumia siku za ibada
Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa ajili ya kuomba msamaha dhidi ya matukio ya
watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Akizungumza jijini Dar es salaam
wakati akikabidhi mabasi kwa Jeshi Mkuu huyo wa mkoa amesema zoezi hilo
litakuwa endelevu baada ya kuanza rasmi jumatatu na kuzitaka taasisi za kidini
nchini kuongoza ibada kwa waumini wao ili kuepuka vitendo hivyo kwa kile
alichokieleza kuwa ni vitendo vya laana.
“Niwaombe, leo ijumaa na
watakaosali jumamosi na jumapili waongoze ibada ya kutubu kama mkoa na kuomba
rehema ya mungu tuishinde hii vita, ndugu zangu niwaambie hili jambo
limelaaniwa tangu kwenye biblia” amesema Makonda
“Juzi nilivyotoa maelekezo
vyombo vikubwa vya habari viliniweka mjadala, Na kuna mtu alinambia mbona
naweka maisha yangu yako hatarini, nikamwambia hapama ila ndiyo nakuwa salama
zaidi mbele ya mungu." Amesema Makonda
Oktoba 31 akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es salaam Paul Makonda alisema "leo zimefika
ujumbe 18972 na hawa wote wanalaani na simu zilizokuwa zinapigwa ni nyingi sana
niwasihi endeleeni kutuma ujumbe ili tuendelee kukomesha biashara hiyo haramu".
"Lakini kwenye hiyo
orodha kuna majina yako 200 lakini kuna baadhi ya watu wamejirudia kwa sababu
wameamua kujitangaza watu hao ni James Delicious, Dida Mtamu, Aunty Miliki,
Abbasi”.Aliongeza Makonda
Makonda azungumzia kutishiwa usalama wake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment