Video vixen, Amber Rutty pamoja na
mpenzi wake ambaye jina lake halijajulikana, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam hii leo kwaajili ya kusomewa mashtaka juu ya
kesi inayowakabili ya kusambaza video zenye maudhui ya ngono mtandaoni.
Akiwa mahakamani hapo, Amber Rutty
amesomewa mashtaka mawili, moja la kukubali kuingiliwa kinyume na maulimbe na
kosa la pili ni kusababisha kusambaa kwa picha za ngono.
Wakati huo huo kijana anayejulikana
kwa jina la James delicious naye amepandishwa mahakamani na kusomewa shtaka
moja la kusambaza video za ngono mtandaoni, ambapo amekataa shtaka hilo.
Ifahamike kuwa iwapo watuhumiwa hao
watakutwa na hatia juu ya makosa yao, kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania watalazimika kwenda jela maisha au adhabu isiyopungua
miaka 30 jela.
Amber Ruty, James Delicious wapandishwa kizimbani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment