Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni leo Jumatano
Oktoba 31, 2018 limemkamata kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe
Kamanda wa polisi wa mkoa huo wa kipolisi, Jumanne
Murilo amethibitisha kukamatwa kwa mwanasiasa huyo ambaye pia ni mbunge wa
Kigoma Mjini na kwamba anahojiwa katika kituo cha polisi Oysterbay
“Ni kweli tumemkamata tunaendelea na mahojiano naye,”
amesema Murilo na alipoulizwa sababu za kumkamata amesema, “Taarifa za kina
tutatoa baadaye.”
Jana, Jeshi la Polisi mkoani Kigoma lilimtaka Zitto
kuwasilisha vielelezo juu ya kauli aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari
Jumapili iliyopita Oktoba 28, 2018 kuwa ana taarifa za wananchi zaidi ya 100
kuuawa katika tukio la mapigano ya wananchi wa jamii ya Wanyantuzu na polisi
wilaya ya Uvinza mkoani humo
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno amesema
tuhuma za mbunge huyo hazina ukweli wowote na kusisitiza kuwa ni upotoshaji
unaofanywa na wanasiasa
Zitto Kabwe akamatwa na Polisi Leo Dar Es Salaam ,Muliro Athibitisha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment