Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma
limemtaka mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kuwasilisha
vielelezo vya madai yake kuwa yametokea mauaji eneo la Nguruka
wilayani Uvinza mkoani humo na watu 100 kupoteza maisha.
Jumapili iliyopita Oktoba 28,2018,
Zitto alizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kudai kuwa
takribani siku 10 zilizopita yalitokea mauaji hayo na taarifa alizonazo ni kuwa
watu zaidi ya 100, wakiwamo polisi walikufa.
Jana Jumanne, Oktoba 30, 2018,
Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Martin Ottieno alizungumza na waandishi wa
habari na kusema tuhuma alizotoa Zitto hazina ukweli wowote.
Alisema hakuna watu 100
waliouawa na kusisitiza kuwa ni upotoshaji unaofanywa na wanasiasa.
“Hakuna watu mia moja waliouawa.
Tunamtaka Zitto aonyeshe vielelezo vya hayo anayosema au aje atuonyeshe
makaburi ya watu hao anaosema wameuawa Kigoma, ”alisema Ottieno.
Kamanda huyo amewataka
wanasiasa kuchukua tahadhali kwa taarifa wanazopewa na watu mbalimbali
kabla ya kuzisambaza ili kuepuka kupotosha jamii.
Zitto aitwa polisi kuthibitisha madai ya mauaji ya watu 100 Kigoma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment