Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameunda kamati
ya watu 15 kwa ajili ya kupambana na watu wanaojihusisha na biashara ya ngono,
huku akiwataka walioweka picha za ngono katika simu kuzifuta kabla ya Novemba
5, 2018
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Oktoba
31, 2018, Makonda amesema kuna mtandao wa watu wanaofanya biashara za ngono
kwenye madanguro na kwenye mitandao ya kijamii ikiwamo makundi ya Whatsapp,
Facebook na Instagram
Amesema kamati hiyo itakayoweka kambi eneo la Mburahati
jijini hapa itajumuisha polisi, wataalamu kutoka Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), Bodi ya Filamu, madaktari na wanasaikolojia
"Kabla ya Jumatatu (Novemba 5, 2018) kila aliyeweka
picha za ngono kwenye simu yake ajitahidi kufuta, nisingependa kuona kiongozi
mtu mashuhuri unakamatwa. TCRA wanaweza kufuatilia mawasiliano kwa kiwango cha
juu hata kwa miezi mitatu nyuma," amesema Makonda
Makonda amesema kama biashara ya ngono itaachwa iendelee
kufanywa inaweza kuhatarisha ustawi wa jamii
"Mkoa wa Dar es Salaam ni kitovu cha maendeleo na
hatuwezi kukwamishwa na watu wachache, tumetangaza vita na watu hawa,"
amesema
Amesema kamati hiyo itaanza kufanya kazi Novemba 5 na tayari
wameshapokea majina ya nyumba zinazotumika kurekodi video za ngono, biashara ya
madanguro
"Tungesema tufanye kimya na kujifanya jambo hili halipo
ni kujidanganya. Jambo hili lipo na linaenda kinyume na maadili ya
Kitanzania," amesema Makonda
RC Makonda Kupambana na Wanaofanya Biashara ya Ngono na Mashoga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment