Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawasaka katibu mwenezi wa
CCM kata ya Mkolani, Zephilin Michael (43) na katibu mwenezi wa chama
hicho kata ya Buhongwa wilaya ya Nyamagana, Hasan Bushangama (43) kwa tuhuma za
kubaka na kulawiti
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema
Michael anatuhumiwa kumlawiti kijana anayekadiriwa kuwa na miaka 16 tukio
lililotokea Oktoba 26, 2018 saa 11:30 jioni katika nyumba moja ya kulala
wageni iliyopo kwenye kata hiyo
Kupitia taarifa yake aliyoitoa leo Jumatano Oktoba 31, 2018,
Shanna amesema mtuhumiwa alimuajiri kijana huyo kuuza kahawa mtaani kisha
alimpangishia chumba katika nyumba hiyo ya kulala wageni ili pindi anapotoka
kuuza kahawa awe anafikia hapo
“Ndipo siku hiyo mtuhumiwa alifika kwenye nyumba hiyo ya
kulala wageni na kumuuliza mhudumu kama kijana wake yumo ndani ya chumba chake
na akaelezwa kuwa yumo, alimfuata humo chumbani huku mhudumu akiendelea na
shughuli zake,” amesema
Amesema baada ya muda mfupi ilisikika sauti ya mtu akipiga
kelele kutoka ndani ya chumba hicho na baadaye watu walipochungulia kupitia
dirishani walimuona mtuhumiwa akimlawiti kijana huyo
“Walimtaka afungue mlango lakini aligoma, baadaye alifungua
na kutoroka na kisha kijana huyo alitoroka lakini wananchi walitoa taarifa
polisi, kwa sasa tunaendelea na msako mkali,” amesema
Katika tukio lingine la Bushangama, anatuhumiwa kumbaka na
kumpatia ujauzito mwanafunzi wa kidato cha pili Sekondari ya Buhongwa mwenye
umri wa miaka 17
Hata hivyo, Shanna amesema mtuhumiwa huyo awali alikamatwa
na kufikishwa kituo cha polisi lakini alidhaminiwa na watu wawili baada ya
kukamilisha masharti yote ya dhamana Julai, 2018
Amesema wakati wakiendelea na taratibu za kumfikisha
mahakamani walipomuhitaji ndipo walipata taarifa kwamba mtuhumiwa ametoroshwa
Aliwataja watu waliomdhamini na wakidaiwa kumtorosha ambao
kwa sasa wanashikiliwa na polisi kuwa ni Mgassa Carlos (42), mkazi wa Bulele na
Jafari Swalehe (57).
Akizungumzia tuhuma za viongozi hao kwa njia ya simu,
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Salum Kalli amesema tayari viongozi hao
wamevuliwa nyadhifa zao
Viongozi CCM wasakwa na polisi kwa kubaka, kulawiti
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment