Zaidi ya wakulima mia mbili kunufaika na elimu ya kilimo biashara.


Happy Lazaro,arusha.

Zaidi ya wakulima mia mbili wanatarajiwa kunufaika na elimu ya kilimo biashara na  kuondokana na kilimo cha mazoea na kuweza kuongeza pato la uchumi zaidi. 

Aidha elimu hiyo tayari  imeanza kutolewa na  Chama  cha Wakulima wa Maua,Matunda na Mbogamboga(TAHA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo Kwa baadhi ya wakulima ambao Ndio wanatarajiwa kuwa mabalozi katika maeneo yao Kwa kuwaunganisha wakulima pamoja na kutoa mafunzo hayo. 

Aidha mafunzo hayo ambayo yametolewa Kwa awamu mbili yalianza tangu febuari mwaka huu hadi sasa hivi ambapo wakulima 12 wamefuzu kuwa wakufunzi wa wakulima wengine baada ya kufikia vigezo vinavyotakiwa. 

Hayo yalisemwa Jana na Meneja mkuu wa maendeleo kutoka Taha, Anthony Chamanga wakati akizungumza katika hafla ya kuwakabithi vyeti wakufunzi hao ambao wataenda kuwa walimu wa wakulima wenzao waliopo vijijini  katika maeneo wanayotokea. 

Chamanga alisema kuwa, wakulima wengi wana uelewa wa kutosha juu ya kulima kisasa, kuzalisha na kutumia teknolojia lakini changamoto kubwa ipo kwenye elimu ya biashara na masoko hali iliyowalazimu kutafuta wadau mbalimbali katika kusaidiana kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo. 

"lengo kubwa la mafunzo hayo ya kilimo biashara ni kuhakikisha kila mkulima anaondokana na kilimo cha mazoea na kupitia wakufunzi hawa tunatarajia kila mmoja afikie wakulima mia mbili kwa mwaka ambapo wakulima hawa wametoka maeneo mbalimbali ikiwemo Arusha, Manyara, Zanzibar, na Kilimanjaro . "alisema Chamanga. 

Kwa upande wa mmoja wa wafadhili wa mafunzo hayo, ambaye ni Mshauri Janneke Beemster kutoka shirika la Trias linalojihusisha na kuwajengea uwezo wakulima na wafugaji alisema kuwa, wameshirikiana na Taha kuhakikisha wanapata wakulima hao ambao waliwapatia mafunzo hayo na Hivi sasa wamekuwa wakufunzi. 

Alisema kuwa, matarajio yao ni kuhakikisha mafunzo hayo yanaleta matokeo mazuri kwa wakulima ili waweze kulima kilimo cha biashara na kuondokana na kilimo cha mazoea walichonacho na kupitia wakufunzi hao wataleta mabadiliko makubwa kwani wao ndio wanategemewa kuwafikia wakulima wenzao kutokana na mbinu walizofundishwa. 

Kwa upande wa Mshauri mwingine kutoka shirika linalosaidia wakulima na wafugaji la Aha, Barbara Pichler alisema kuwa, wamekuwa wakishirikiana Kwa pamoja kuwezesha wakulima na kuongeza ujuzi katika ujasiriamali, na kuwa na uwezo zaidi katika eneo lao la biashara. 

Baadhi ya wakulima waliohitimu mafunzo hayo kutoka mkoani Kilimanjaro , Hashimu Abdalah  na Clemence Makundi kutoka Arumeru walisema kuwa, wameweza kujifunza mbinu mbalimbali za kilimobiashara na kupata uelewa mkubwa wa mambo ambayo walikuwa hawayafahamu hapo awali, hivyo wataenda kuwa mabalozi wa wakulima wengine katika maeneo yao. 


Zaidi ya wakulima mia mbili kunufaika na elimu ya kilimo biashara. Zaidi ya wakulima mia mbili kunufaika na elimu ya kilimo biashara.    Reviewed by KUSAGANEWS on October 31, 2018 Rating: 5

No comments: