Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsi wazee na watoto Mh Ummy Mwalim amepiga marufuku hospitali zote nchini utozaji wa fedha kwa wahanga wa vitendo vya ukatili pamoja na kuwataka wakuu wa shule zote za msingi na sekondari nchini kuhakikisha wanapeleka taarifa za kila robo mwaka kwa makamishina wa elimu kuhusu mimba na ndoa za utotoni.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam katika Kongamano la kitaifa la kujadili namna ya kudhibiti ukeketaji ,mimba na ndoa za utotoni amebainisha kuwa katika kupambana na mimba na ndoa za utotoni ni vyema wakuu wa shule zote za msingi na sekondari wakazingatia kutunza na kupeleka taarifa hizo.
Aidha ameongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la UNCEF mwaka 2017 nchi ya Tanzania inashika nafasi ya 11 kati ya nchi 20 Duniani zenye kiwango kikubwa cha mimba na ndoa za utotoni huku asilimia 37 huolewa kabla ya umri na kwa mwaka 2016 ikiwa ni asilimia 36 .
Kwa upande wake mkuu wa Dawati la jinsia makao makuu ya polisi CP MARRY NZUKI amesema jeshi la polisi lipo tayari kushirirkiana na wadau katika kudhibiti ukeketaji,mimba na ndoa za utotoni na mpaka sasa kuna madawati 420 nchi nzima ya kudhibiti ukatili dhidi ya mtoto wa kike.
Clip 2…. Nzuki
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa shinyanga Bi,Zainabu Telack amesema kwa mwaka jana mkoa huo ulikuwa na mimba 259 za utotoni lakini wamefanikiwa kuwabana wakuu wa shule ili kuhakikisha wanasimamia mahudhurio ya wanafunzi pamoja na wazazi kuwapatia elimu.
Naye mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima amebainisha kuwa ukatili umefichwa katika jamii huku mila desturi na tamaduni zimekuwa na nguvu na kushikilia vitendo hivyo huku viongozi wakishindwa kueleza ukweli jamii kwa kuogopa kukosa nyadhifa za uongozi .
Aidha Mikoa inayoongoza kwa mimba za utotoni nchini ni Shinyanga ,Tabora mara ,Dodoma ,lindi, Mtwara,na manyara hali ambayo inasabibihsa mtoto kukosa masoma na kuendelea kuwa masikini na kuendelea kuwa tengemezi huku umasikini katika familia,na kuendeleza kwa mila ukichangiakwa kiasi kikubwa mimba na ndoa za utotoni
Waziri Ummy Apiga marufuku wahanga wa ukatili wa kijinsIa kutozwa pesa za matibabu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 09, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 09, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment