Serikali imepiga marufuku madaktari kuwaandikia wagonjwa dawa kwa
kutumia majina ya kampuni badala yake watumie majina ya kitaalamu.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Oktoba 10, na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile, katika
kuangalia mfumo wa upatikanaji dawa na vifaa tiba nchini.
Amesema tabia ya madaktari kuandika dawa kwa kutumia majina hayo ya
kampuni kumesababisha wagonjwa kukosa dawa na licha ya kuwapo kwa dawa nyingine
zenye uwezo wa kutibu sawa na hizo.
“Dawa zinazotumika hapa nchini ni sawa na zile zinazotumika katika nchi
nyingine duniani, kwa hiyo kutoa dawa China, India, Marekani au Ulaya ni
utofauti wa gharama.
“Kwa mfano mimi ni daktari nikikuandikia ukanunue soda ukikuta soda
yoyote utapona ila nikikwambia ukanunue Cocacola lazima uipate hiyo.
“Kwa hiyo wawaAndikie wagonjwa dawa kwa majina ya asili kwa sababu
ukimwandikia mgonjwa panadol ni kumtaka lazima anunue dawa hiyo hata kama kuna
dawa nyingine hawezi kupewa,” amesema Dk. Ndugulile.
Serikali yapiga marufuku madaktari kuandika dawa kwa majina ya kampuni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 10, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 10, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment