Mjadala waibuka Bungea la EALA

Mjadala mkali umeibuka katika bunge la
 Jumuia ya Afrika Mashariki mara baada ya mbunge wa bunge hilo Mathias Kasamba kuleta hoja binafsi ya uharibifu wa misitu pamoja na benki ya Maendeleo ya Afrika mashariki ambapo nchi baadhi ya wananchama hadi leo hawana hisa hata moja katika benki hiyo.

Akitoa hoja hiyo Mhandisi Mohammed Mnyaa mbunge kutoka nchini Tanzania amesema kuwa nchi Tatu zilizokuwepo awali kwenye muungano wa jumuiya hiyo ambazo ni Kenya,Uganda na Tanzania ndizo ambazo bado zina hisa pekee na benki hiyo ambapo haiendeshwi kwa misingi ya protokali ya jumuiya hiyo.

"Baada ya jumuia ya pili kufufuliwa na kuanza kufanyakazi ilielezwa kuwa benki hiyo ni Mali ya Jumuia ya afrika mashariki,lakini utendaji wake hako katika protokali ya Jumuia ya Afrika mashariki tunachoomba baraza la mawaziri wa Jumuia hiyo wafuatilie jambo hilo"Amesema Mnyaa.

Aliambia bunge hilo kuwa benki hiyo ya maendeleo ilikuwepo kabla ya kuvunjwa kwa jumuiya hiyo ila protokali ya uundwaji wa jumuiya hiyo mwaka elfu mbili unaitambua benki hiyo kama moja ya taasisi ya jumuiya hiyo.

Benki hiyo inatakiwa kuwa taasisi kamili ya jumuiya hiyo ifikapo desemba mwaka huu kwani mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo amehakikisha kuwa wanalichukuwa na kulifanyia kazi.

Amesema kuwa jambo la pili lililojadiliwa katika bunge hilo ni linalohusu uharibifu wa Misitu kwa nchi wanachama wenzetu isipokuwa Nchi ya Rwanda ambayo inafanya vizuri nkatika mutunzaji wa misitu.

“Jumuiya ya Afrika mashariki ilipovunjika nchi ziligawana mali ila benki hiyo na ziwa victoria basin ndizo mali zilizobakia ndani ya jumuiya hiyo benki hiyo ambayo makao makuu yapo Uganda imekuwa haijiendeshi kama taasisi ya jumuiya hiyo na imeweza kuwapa hisa hadi wageni tofauti na protokali” aliliambia Mhandisi Mnyaa.
Mjadala waibuka Bungea la EALA Mjadala waibuka Bungea la EALA Reviewed by KUSAGANEWS on October 09, 2018 Rating: 5

No comments: