Halmashauri nchini zimeagizwa kuanza kutoa vibali vya ujenzi
ndani ya siku tatu, huku maofisa mipango miji wakitakiwa kusimamia agizo hilo
Pia, imesisitiza kuwa kazi ya urasimishaji maeneo
yaliyojengwa kiholela lazima iendelee na haitakiwi kuambatana na ubomoaji wa
nyumba za watu
Maagizo hayo yalitolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipokuwa akifungua mkutano wa Bodi ya
Wataalamu wa Usajili Mipango Miji jijini Dodoma jana
Lukuvi alisema vibali vya ujenzi wa nyumba katika maeneo
mbalimbali nchini ni lazima vitolewe ama katika maeneo yaliyopangwa au
yasiyopangwa na kwamba, jambo la msingi inalotaka Serikali ni kuwa na majengo
yaliyopangiliwa vizuri. “Ucheleweshwaji wowote wa utoaji kibali lazima mhusika
afahamishwe sababu,” alisema Lukuvi
Alisema lengo la maofisa mipango miji kupewa mamlaka ya
kutoa vibali vya ujenzi badala ya wakuu wa idara wa halmashauri linatokana na
baadhi ya maeneo hayo kusimamiwa na watu wasiokuwa na taaluma ya sekta husika,
jambo linaloweza kuvuruga upangaji wa miji
Waziri Lukuvi alitaka nakala za vibali vya ujenzi
zitakazotolewa zipelekwe pia katika ofisi za maofisa watendaji wa mitaa kwa
kuwa wanapaswa kufahamu kinachoendelea katika maeneo yao. Pia, aliagiza bodi za
usajili wa mipango miji kuandaa mwongozo utakaowasaidia watendaji wa mitaa kuwa
na ufahamu katika kusimamia mipango ya uendelezaji miji, jambo litakalosaidia
kuepuka ujenzi holela kwa baadhi ya maeneo
Kuhusu urasimishaji maeneo yasiyopimwa, alisema licha ya
kazi hiyo kufanyika nchi nzima, hakuna nyumba itakayovunjwa na kutaka kampuni
zote zitakazotaka kufanya kazi ya urasimishaji ardhi kutuma maombi kupitia
ofisi za wilaya
Akizungumza katika mkutano huo, mtafiti na mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Ardhi (Aru), Salfonce Kesi alisema kwa sasa mambo mengi ya upangaji
miji nchini hayaendi vizuri kutokana na mipango kufanywa na watu wasio na
taaluma hiyo. Kesi alisema lazima suala la mipango miji katika maeneo lianze na
mipango mingine ya huduma za jamii
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Mipango Miji, Profesa
Wilbert Kombe alisema wameanza kuchukua hatua kuhakikisha taaluma ya mipango
miji inakuwa na wataalamu wanaozingatia sheria
Waziri Lukuvi aagiza Halmashauri Kutoa vibali vya ujenzi vitolewe ndani ya siku tatu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment