Mkuu Wa Wilaya Ya Arumeru
Mhe.Jerry Muro Wakati Wa Ufunguzi Wa Kikao Cha Ushauri Cha Wilaya Hiyo
(DDC) Ameeleza Kuwa Wilaya Hiyo Imejikita Kwenye Dira Na Mwelekeo
Wa Taifa Hususani Katika Uchumi Wa Viwanda.
Mhe.Muro
amefafanua kuwa katika kuongeza kasi ya kuelekea uchumi wa viwanda
Wilayani humo utatuzi wa changamoto mbalimbali ambazo ni vikwazo kwenye
uwekezaji wa viwanda ikiwemo rasilimali ardhi umepewa kipaumbele
"ardhi
ni rasilimali muhimu katika uchumi wa viwanda lazima tuwe na ardhi isiyo na
migogoro ili kuvutia na kuimarisha uwekezaji wa viwanda katika wilaya
yetu."amesema Mhe. Muro.
Aidha
mwezi Septemba mwaka huu, ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya ya Arumeru
iliendesha zoezi la utatuzi wa kero za wananchi lililokuwa na mafanikio makubwa
kwani mamia ya wananchi walipata utatuzi wa kero zao ,
zoezi hilo la utatuzi
wa kero za Wananchi lililopewa jina la "PAPO KWA PAPO"
lilifanyika kwa kuzingatia sheria ambapo wanananchi waliokuwa na
kero mbalimbali walifika ofisi ya Mkuu wa wilaya na kusikilizwa na
jopo la wanasheria pamoja na wataalamu kutoka kitengo cha ardhi, ustawi wa
jamii na Polisi hivyo wananchi walipewa ushauri wa kisheria pamoja na
msaada wa ngazi zinazofuata kwa utatuzi zaidi.
Mkuu
huyo wa Wilaya amewataka watumishi wa serikali kuanzia ngazi ya Vijiji wilayani
humo kuwajibika ipasavyo kwa kuwa makini kwenye utendaji wao sambamba na kutoa
huduma kwa wakati," msiwatese wananchi kutumia nauli na muda kuja kutoa
kero katika ofisi yangu ambayo ingeweza kupata utatuzi katika ngazi ya
kijiji,"Amesema Muro
Aidha
Mhe.Muro amehitimisha mazungumzo yake kwa kuwakaribisha wadau wa kikao hicho
kutoa ushauri na mawazo yatakayoweka mipango, mikakati na maazimio
yatakayo waletea wananchi wa Arumeru maendeleo na kudumisha Amani iliyopo.
DC MURO Tumejikita katika Uchumi wa Viwanda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment