Rc Gambo Ni Heri Arusha Kuwa wa Mwisho Kuliko Udanganyifu


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa mkoa huo hata kama utakuwa wa mwisho katika ufaulu kitaifa lakini suala la wizi wa mitihani lipigwe vita kwa nguvu zote sanjari na udanyanyifu katika masomo kwani inawajenga wanafunzi kuwa sio waadilifu siku za usoni.
Gambo ameyasema hayo wakati wa mahafali ya Kidato cha nne kwa shule zote za serikali na binafsi za jiji la Arusha  zilizofanyika kiwilaya katika uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini hapa na kuwataka viongozi wote katika mkoa huo kupiga vita udanganyifu wowote katika masuala
Aidha kwa upande wake Afisa Elimu jiji la Arusha Valentine Makuka amesema kuwa halmashauri ya jiji hilo iliona kuna baadhi ya wanafunzi hawana uwezo wa kumudu gharama za kusherehekea mahafali hivyo kuja na utaratibu huo ambao utasaidia watoto wasio na uwezo nao kujiona ni sehemu ya utaratibu huo.
Hata hivyo viongozi wa dini kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wanaunga mkono serikali kufanya mahafali hayo ya pamoja na utaratibu huo watahimiza kwa waumini wao kuweza kuchangia katika elimu kwani ni sehumu ya urithi mzuri kwa jamii sanjari na kuhimiza kujitolea kusaidia wanafuzni hao kuweza kujenga taifa lenya maadili.
Rc Gambo Ni Heri Arusha Kuwa wa Mwisho Kuliko Udanganyifu Rc Gambo Ni Heri Arusha Kuwa wa Mwisho Kuliko Udanganyifu Reviewed by KUSAGANEWS on October 31, 2018 Rating: 5

No comments: