Na
KUSAGA,Arusha.
Vijana nchini
wametakiwa kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo imekua ikitumika
kufanya uhalifu wa kimtandao pamoja na kuchangia kuporomoka kwa maadili ya
vijana wanaoiga tamaduni za nchi za nje zisizofaa.
Akizungumza
katika Kongamano la Maadili liliofanyika Wilaya ya Karatu ,Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Arusha Dk. John Pallangyo amesema kuwa vijana
wanapaswa kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao pamoja na kuhakikisha kuwa
wanalinda maadili ya Tanzania na kuchangia maendeleo kwenye jamii na taifa.
Mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo Wilaya ya Karatu Peter Mmasy amesema kuwa jumuiya hiyo ina jukumu
la kusimamia malezi,maadili ya jamii na kuwataka Wazazi kutimiza wajibu wao kwa
kuwalea vyema vijana.
Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa mkoa wa Arusha kupitia CCM, Cylius Daniel Mlekwa amesema
kuwa licha ya kusisitiza maadili pia vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele
katika kupiga vita rushwa ili kuwa na jamii bora.
Kwa Upande
wake Kijana aliyeshiriki katika Kongamano hilo Elitumaini Rweyemamu amesema
maadili na nidhamu ni nguzo ya mafanikio kwa vijana hivyo vijana hawana budi
kusimamia vyema maadili ya kitanzania ambayo yamegubikwa na utandawazi.
VIJANA Epukeni Matumizi mabaya ya Mitandao ya Kijamii
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment