Wananchi wa jiji la
Arusha wametakiwa kuchangamkia fursa zinazotolewa na mashirika ya kimataifa
yanayofanyakazi ndani ya jiji hilo lengo likiwa ni kuangalia fursa zinazotokana
na mashirika hayo kukuza vipato vyao na uchumi wa jiji hilo.
Akizungumza na
vyombo vya habari jijini Arusha Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Kalist
Lazaro amebainisha kuwa Maonyesho hayo Pili ya mashirikia ya kimataifa
yanayojulikana kwa jina la (Internation Organization Arusha open
day)yanatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya tarehe 3 mwezi novemba katika
viwanja vya lakilaki nje kidogo ya jiji la Arusha.
Amesema kuwa
wananchi watatakiwa kuwa na vitambulisho kuweza kushiriki maonyesho hayo ambayo
ni mara ya pili yanafanyika na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa mambo ya nje
kikanda na Afrika mashariki Balozi Agastine Mahiga na usafiri utakuwepo maeneo
yote ya jiji hili na kiingilio ni bure
Amesema kuwa
maonyesho hayo ambayo yanafanyika katika majiji matatu tu ya Durban New York na
Arusha mwakani kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam na hivyo kutoa fursa
kwa taasisi mbali mbali za kimataifa ambazo zipo hapa nchini kuweza
kushirikiana na wananchi katika kuonyesha shughuli wanazozifanya hapa nchini
lengo likiwa ni wananchi kujua shughuli wanzozifanya na fursa gani wanaweza
kushirikiana.
Amesema kuwa
maonyesho hayo ambayo mwaka jana yalikuwa ya majaribio hivyo kuwataka wananchi
wengi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonyesho hayo ikiwa ni sehemu ya
kukutana na kuweza kujua mashirika hayo yanafanya nini na yapo eneo gani kuweza
kujua fursa walizonazo.
Maonyesho ya Pili Kimataifa Kufanyika Jiji la Arusha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment