Watumishi 9 mbaroni kwa Kufoji Risiti za EFDs



Watumishi tisa wa soko la kwa Sadala  akiwemo mkuu wa  soko ilo Bw. Joseph Akyoo  wamekamatwa na  maafisa wa TAKUKURU kwa kushirikinana na  jeshi la polisi katika mkutano wa hadhara wakituhumiwa  kuharibu mashine za kutolea risiti  za EFDs na kutumia risiti bandia kukusanya ushuru katika soko hilo  hali iliyotajwa  kuisababishia hasara serikali

Watumishi  hao wa  soko hilo wamekamatwa baada ya kuibuka kwa tuhuma kutoka kwa maelfu ya wafanyabiashara  mbele ya mkutano na kudai kuwa wamekuwa wakipewa risiti feki za kuandika kwa mkono na kuchukua fedha ambazo hazifiki halmashauri lakini pamoja na kutoa fedha hizo bado mazingira ya soko ilo bado ya uchafu uliyokithiri

Baada ya  kusikia tuhuma hizo kutoka kwa wafanyabiasha  mkuu wa wilaya ya Hai Bw.Lengai Ole Sabaya akatoa maelekezo ya serikali  na kutaka watuhumiwa washikiliwe ili kupisha uchunguzi

Mkurugenzi  wa halmashauri ya wilaya ya  Hai Yohana Sinto amesema matukio ya ubadhilifu  wa risiti unachangia kuikoseshaserikali mapato  huku akiahidi kutatua tatizo sugu la uchafu  ulilokithiri kwenye soko hilo.




Watumishi 9 mbaroni kwa Kufoji Risiti za EFDs Watumishi 9 mbaroni kwa Kufoji Risiti za EFDs Reviewed by KUSAGANEWS on October 06, 2018 Rating: 5

No comments: