Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa Jimbo lake kutoulizia Milioni 50 za kila kijiji ambazo ziliahidiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Mbunge huyo Serikali
imetoa milioni 800 kwa ajili ya kujenga hospitali za Tarafa katika baadhi ya
kata kwenye jimbo hilo pamoja kupatiwa bilioni 2 kwa ajili utekelezaji miradi
ambayo itawanufaisha wananchi wote.
Katika mkutano wake wa hadhara
jimboni kwake, Mwigulu amesema “nisikilizeni wana Iramba, Serikali imetupatia
milioni 800 za kujenga hospitali za Tarafa Kinampanda na Ndago, tumepata zaidi
ya bilioni 2 kujenga daraja tarafa ya Shelui, tumeshapata zaidi ya bilioni 2
kwa ajili ya maji.
Aidha Mwigulu Nchemba “hizi ni
huduma za watu wote na hazikuwepo kwenye ilani, ni upendo na maono ya Rais.
Tumshukuru mhe Rais wetu mpendwa badala ya kuulizauliza milioni 50. Na kwa
Vikundi tutaendelea kuwapa asilimia kumi ya mapato ya ndani."
Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2015 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kupitia
ilani ya Chama Cha Mapinduzi aliahidi kutoa milioni 50 kwa kila kijiji kwa
nchini kwa ajili ya maendeleo.
Mwigulu Nchemba aibuka na milioni 50
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment