Meya wa Manispaa ya Ubungo kupitia
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Boniface Jacob amesema anapenda
nafasi ya Ukuu wa Mkoa na Ukuu wa wilaya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
lakini hawezi kuhamia chama hicho kwa kile alichokidai atakuwa amewasaliti
wananchi wake,
Akizungumza Meya Boniface Jacob amesema katika vitu
ambavyo hatamani kuvisikia kwa mtu yeyote ni kwamba yeye binafsi ana
mipango ya kuhamia CCM na kusema kauli hiyo ni inalenga kumdhalilisha.
“Kwa mfano mimi nina maisha magumu
napenda Ukuu wa Mkoa, Ukuu wa Wilaya shida ni kwamba nitafata vitu vizuri
lakini sitakuwa na amani ya roho sababu nitawasiliti watanzania wenye maisha
magumu, hicho ndio kinanifanya nisiwe upande wa CCM,” Amesema Meya wa Ubungo
Boniface Jacob.
Kuhusiana na mapigano ya hivi
karibuni yaliyotokea kwenye Uchaguzi wa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala amesema
tukio hilo limemkumbusha uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji ambapo Meya huyo wa Ubungo
alishikana mashati na Meya wa Temeke Abdallah Chaulembo.
“Unajua wananchi wanapaswa kujua
kuwa vyama vya upinzani huwa vinapata tabu sana kwenye uchaguzi hapa nchini
lakini niwaambie hatutakata tama, tutaendelea kutetea haki zetu.” Ameongeza
Meya wa Ubungo Boniface Jacob.
“Nina maisha magumu napenda ukuu wa mkoa” - Meya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment