|
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Simanjiro mkoani Manyara, Awadhi Omary amemkaribisha aliyekuwa mbunge
Simanjiro (Chadema), James Millya ndani ya chama hicho tawala
Akizungumza leo jioni Jumapili
Oktoba 7, 2018, Awadhi amesema hatua hiyo ni faraja kwa CCM hivyo
wanamkaribisha kwa mikono miwili kwani jimbo hilo halitakuwa kwenye mikono ya
Chadema tena
Amesema ni jambo la heri kuona mtu
akikimbia kwake anakuja kwako endapo atakuja kwa nia nzuri ni furaha kubwa
kwako
"Hata hivyo, suala la
kugombea ubunge wa Simanjiro litasubiri vikao halali juu ya Millya endapo
atapitishwa au laa," amesema Awadhi
Diwani wa Endiamtu (Chadema),
Philemoni Oyogo amesema amesikitishwa mara baada ya kupata taarifa kuwa
Millya amejiuzulu nafasi hiyo na amehamia CCM
Oyogo amesema yeye ataendelea kuwa
diwani wa Endiamtu kupitia Chadema na hayupo tayari kujiuzulu nafasi hiyo na
kujiunga na CCM
Diwani wa Mirerani (Chadema),
Thomas Yohana amesema hawezi kuzungumza chochote zaidi kwani Millya ametumia
demokrasia yake kama Mtanzania kujiunga CCM
"Siwezi kuzungumza chochote
yeye ametumia uamuzi wake ila mimi siwezi kuhama Chadema eti kwa sababu ya
kumuunga mkono yeyote nitaendelea kuwa diwani wa Mirerani kwa tiketi ya
Chadema," amesema Yohana
Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa
wilaya ya Simanjiro wamepongeza hatua ya Ole Millya kuondoka Chadema na
kujiunga na CCM
Mkazi wa mtaa wa Kazamoyo, Mustafa
Kabota amesema Millya alienda Chadema kwa ajili ya kutafuta mabadiliko lakini
amerudi baada ya kuona hakuna mabadiliko yoyote na kuamua kurudi CCM
"Nawaomba madiwani wa kata ya
Mirerani na Endiamtu ambao nao wapo Chadema warudi CCM kwani huko Chadema
hakuna wanachokifanya," amesema Kabota
Mkazi wa Mirerani, Hassan Juma
amesema hata ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite uliwekwa ili
kuwakomoa wananchi wa eneo hilo baada ya kumchagua Millya na madiwani wa
Mirerani na Endiamtu
"Nadhani sasa hivi
tutaruhusiwa kupita ndani ya ukuta kwani haya mambo ya kisiasa yalitugharimu
ila kwa sababu jamaa amemuunga mkono mzee sasa mambo yatakuwa safi,"
amesema Juma
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa
Manyara, Gervas Sulle amesema hana taarifa ya Millya kujiuzulu ubunge na
kuhamia CCM
"Sina hizo taarifa rasmi za
Millya ila Katiba inamruhusu ni uhuru wa mtu hao wanaosema tumepata pigo
hakuna pigo tulilolipata," amesema Sulle
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2015, Millya alimshinda mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka na pia
madiwani sita wa Chadema walishinda kwenye kata za Mirerani, Endiamtu,
Naberera, Loiborseret, Ruvu Remit na Loiborsoit
Katika mkoa wa Manyara Chadema
ilishinda majimbo mawili ya Simanjiro na Babati Mjini linaoongozwa na Pauline
Gekul wa Chadema kati ya majimbo saba
|
CCM Simanjiro wamkaribisha Millya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment