Mbunge wa
Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema aliyekuwa mbunge wa Simanjiro,
James Millya alihama siku nyingi ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini
Akizungumza na
Mwananchi leo Jumapili Oktoba 7, 2018 muda mfupi baada ya barua ya Millya
kusambaa kuwa amejizulu, Lema amesema hajashtuka wala kushangazwa na uamuzi huo
wa kuamua kurejea CCM
“Millya
alikuwa ameshahama muda mrefu Chadema, ukiangalia matendo, mienendo yake, sisi
tulishamwona amehama,” amesema
Lema ambaye
amekiri ni rafiki wa Millya na alihusika katika kumpokea wakati akihamia
Chadema mwaka 2013 amesema,
“Kilichonishangaza ni Millya kuchelewa kwenda CCM.
Millya alipaswa kuwa mtu wa kwanza kabla ya madiwani na wabunge kuhamia lakini
amekuwa wa mwisho ndicho kinanishangaza
“Bado
sijaelewa hao wanaosema wanakwenda kuunga mkono, utaungaje mkono juhudi kukiwa
na matatizo mengi, demokrasia inafinyangwa, waandishi wanatekwa, watu
wanapotea, uchumi mgumu, ajira ni tatizo,” alihoji Lema.
Unapokuwa
mwanasiasa wa upinzani unapaswa kujua unapigania si masilahi yako bali ya
wajukuu na vizazi vijavyo lakini kwa Millya ameamua kujinufaisha yeye binafsi,”
amesema.
Lema: Millya alihama siku nyingi Chadema
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment