|
Mbunge wa Simanjiro (Chadema),
James Millya amejiuzulu nafasi hiyo na uanachama wa chama hicho kikuu
cha upinzani huku akitangaza kurejea CCM
Millya ambaye alimshinda
Christopher Ole Sendeka (CCM) katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 ametangaza
uamuzi huo leo, Jumapili Oktoba 7, 2018 katika barua yake kwenda kwa Spika wa
Bunge Job Ndugai
Katika barua hiyo, Millya amesema
amekuwa mwanachama wa Chadema kwa miaka sita baada ya kuhama CCM uamuzi
aliouchukua kutokana na kiu ya kuitafuta haki wakati huo na jukwaa ambalo
angeweza kupaza sauti kwa misingi ya hoja na kupambana na rushwa na ufisadi
“Naandika barua hii nikiwa na
uhalisia mwingine kabisa, kila mtu atakuwa shuhuda nimekuwa si mtu wa siasa
za jukwaani kwa miaka hii mitatu.”
“Ni dhahiri kwamba nimepoteza
imani na kukosa amani, mahali nilipo sipaoni tena kama ni jukwaa la kunituma
na kuhamasisha kuwaletea maendeleo wana Simanjiro,” amesema Millya
Amesema chama cha siasa kinapaswa
kuwa taasisi yenye mwelekeo wa kiitikadi na inayowatuma wawakilishi akiwemo
yeye kuwahamasisha wananchi kushirikiana na Serikali kutafuta na kuleta
maendeleo na si vinginevyo
“Ukweli ambao nimeuishi umekuwa
mchungu na kinyume na matarajio yangu. Najua siasa za siku hizi msingi wake
si siasa safi na zinatufanya ukiwa mbunge wa upinzani kila jambo unapinga
hata pale kazi nzuri imefanyika ni dhambi kuunga mkono na kutoa hamasa ya
kuongeza juhudi.”
“Siasa hizi hazina afya kwa Taifa
letu na wananchi wa Simanjiro, licha ya changamoto za hapa na pale lakini
ukweli usiopingika Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa sana chini ya Rais
John Magufuli,” amesema Millya
Millya amesema kinachosikitisha
badala ya kusimama pamoja katika mafanikio ya Rais Magufuli na kumsaidia kwa
kumpa mbadala wa hoja na mipango, matokeo yake upinzani umekuwa na kazi ya
kubeza na kuponda chochote kinachofanyika
Ameongeza bahati mbaya hata pale
yanayofanyika na kugusa na kubadilisha maisha ya Watanzania, alisema hizo si
siasa alizokuwa akizitarajia upinzani izifanye katika Taifa ambalo lina kazi
kubwa la kukombolewa kiuchumi
“Kipindi hiki nikiwa huru
nimejipanga kufanya kazi na wadau mbalimbali wakiwemo wabunge wa maeneo ya
wafugaji na viongozi wa Serikali ili kutoka na mapendekezo ya utatuzi wa
kudumu wa changamoto za wavuvi, wakulima na wafugaji na namna ya kuratibu
matumizi bora ya ardhi na maeneo yao,” amesema
Wabunge wengine sita wa upinzani
waliohamia CCM ni; Maulid Mtulia (Kinondoni-CUF), Dk Godwin Mollel (Siha-
Chadema), Julius Kalanga (Monduli- Chadema), Mwita Waitara (Ukonga- Chadema),
Zuberi Kuchauka (Liwale- CUF), Marwa Chacha (Serengeti) huku Lazaro Nyalandu
(Singida Kaskazini) akitoka CCM kwenda Chadema
|
James Millya Akimbilia CCM leo kutoka CHADEMA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment