|
Dereva wa basi la abiria nchini
India amefukuzwa kazi baada ya kumruhusu nyani aendeshe basi hilo
Dereva huyo amefukuzwa ingawa
hakuna hata abiria mmoja aliyekuwa kwenye basi hilo ambaye alilalamikia
kitendo cha dereva huyo kumruhusu nyani kuendesha basi hilo
Hata hivyo baada video ya nyani
huyo aliyekuwa ametulia huku akiwa ameshikilia usukani wa basi hilo kusambaa
mitandaoni, waajiri wake walimchukulia hatua ya kumfukuza
Hata hivyo hatua hiyo ya waajiri
kumfukuza kazi dereva huyo haijawafurahisha watumiaji wa mitandao ambao
walifurahishwa na video hiyo
"Vizuri sana, kwa nini
mumfukuze . Angepewa onyo na aambiwe asirudie, mmoja wa wasomaji aliandika
katika ukurasa wake wa Twitter
Kwa mujibu wa walioshuhudia, nyani
alipanda gari na abiria mwingine lakini akakataa kukaa nyuma bali akachagua
kiti cha dereva
Dereva huyo aliyefahamika kwa jina
la Prakash, ambaye alionekana kutotilia maanani sana suala hilo, alimruhusu
nyani kukaa kwenye usukani huku wakiendelea na safari
Inadaiwa kwamba nyani huyo
alipofika kwenye kituo chake alishuka na kumuacha dereva akiendelea na safari
yake.
|
Dereva afukuzwa kazi kwa kumruhusu nyani aendeshe basi la abiria
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment