Waziri wa Maji na Umwagiliaji Professa Makame Mbarawa
amezindua Dira ya maji ya malipo kabla (prepaid meter) jijini Mwanza leo Agosti
15 na kuwataka watendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa)
kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa huduma hiyo
Amezindua huduma hiyo kwa kufunga mita hiyo nyumbani kwa
mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dk Philis Nyimbo akiwa ni mteja wa pili kufungiwa
mita hiyo akitanguliwa na mkuu wa mkoa huo John Mongella
Amesema kuzindua mfumo huo ni jambo moja lakini hautakuwa na
maana endapo wananchi wanaolengwa kama hawatapewa elimu jinsi ya kujiunga na
kufahamu umuhimu wa matumizi yake.
Ameagiza mamlaka hiyo
kuzifungia kwanza taasisi za serikali, mahoteli na viwanda ambapo mfumo huo
ukiunganishiwa wateja wengi utainua mapato yao
"Tumezindua mfumo huu leo, ni mzuri lakini tunapaswa
kutoa elimu kwa wananchi ambao ndio wateja wetu ili wawe na uelewa, mkifanya
hivyo ninaamini kuna mabadiliko makubwa yatapatikana," amesema
Meneja mifumo ya mawasiliano wa Mwauwasa, Alena Kalinjuna
amesema kwa sasa mamlaka imeshanunua mita 117 za malipo kabla zenye ukubwa
tofauti ambazo zitafungwa kwa awamu kwa wateja mbalimbali
Amesema miongoni mwa faida za mfumo huo ni pamoja na
kuongeza mapato, kupunguza kiasi cha maji yanayopotea na kupunguza udanganyifu
Amesema kwa mwaka wa fedha 2019/20 wanalenga kuwafungia mita
hizo wateja 500 wakianza na taasisi za serikali
Mkoa wa Mwanza una jumla ya wateja wa 75,629 wanaohudumiwa
na Mwauwasa huku malengo yakiwa ni kufikisha wateja 100,000 ifikapo Juni 2019
Waziri Mbarawa azindua dira ya maji ya malipo kabla
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment