Serikali
imekutana na wadau wa sekta ya viwanda kujadili kuadimika kwa saruji, huku
inayopatikana ikiuzwa bei ya juu
Kikao hicho
kinachoongozwa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella
Manyanya kimehudhuriwa na wazalishaji wa saruji na wa makaa ya mawe,
wasafirishaji na wadhibiti.
Akizungumza katika mkutano huo unaofanyika
jijini Dar es Salaam leo Agosti 15, 2018 Manyanya amewataka wazalishaji wa
saruji kueleza uwezo wao wa uzalishaji
Naibu waziri
pia amewataka kueleza sababu za kusimamisha uzalishaji ghafla na kwa viwanda
vyote
"Imetushitua
kuona saruji imepotea sokoni na kupanda bei ghafla, tena viwanda vyote.
Tukasema hapo ni zaidi ya masuala ya kiufundi, kwa hiyo tumewaita kuwasikiliza
tujue tatizo ni nini ikiwezekana leo tutoke na uamuzi,” amesema Manyanya
Naibu waziri
amesema sasa kuna fursa nyingi za soko la saruji kupitia miradi inayotekelezwa
na Serikali.
Amesema hiki ndicho kipindi cha kuongeza
uzalishaji lakini anashangazwa kuona saruji imeadimika na bei imepanda
Serikali yajadili kuadimika kwa Saruji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment