Kada wa Chadema, Fred Lowassa leo Agosti 15 amejiondoa
kwenye kinyang’anyiro cha wanaowania kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge
jimbo la Monduli
Baada ya kujiondoa, Chadema kimempitisha diwani wa kata ya
Lepurko, Yonas Masiaya Laizer kuwania ubunge wa jimbo hilo
Fred, ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa
alichukua fomu ya kuwania ubunge jimbo hilo wiki iliyopita
Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Julius Kalanga, alijiuzulu
uanachama wa Chadema na ubunge na kuhamia CCM. Kalanga ameshateuliwa na CCM
kugombea ubunge jimbo hilo.
Akizungumzia uamuzi
wa Fred, katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Amani Golugwa alisema baada ya
kushauriana, vikao vya uteuzi vilikubali kuondoa jina lake
"Ni kweli nathibitisha kuwa ameomba kwa sasa si wakati
muafaka licha ya kuwa alionesha nia awali na wananchi wengi walimuunga mkono,
hivyo chama kimekubali maombi yake na kimempitisha mgombea
mwingine,"amesema Golugwa
Fred Lowassa ajiondoa kuwania ubunge Monduli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 15, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment