NEC yajibu taarifa ya ubalozi wa Marekani kuhusu Uchaguzi Mdogo


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi juu ya madai ya Ubalozi wa Marekani kuhusu uchaguzi mdogo wa Agosti 12

Katika taarifa iliyotolewa leo Agosti 15, 2018 NEC imeutaka ubalozi huo uthibitishe  inachokieleza juu ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu na kata 36 ikisema uchaguzi mdogo huwa hauna waangalizi wa kimataifa na kuhoji ubalozi huo umetoa wapi taarifa hizo na hayo ulioyaona ni kwa kutumia utaratibu upi na sheria ipi

“Katika Jimbo la Buyungu mgombea wa ubunge mmojawapo (Chadema) alijitokeza  kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii akaeleza hisia zake na kusema bayana kuwa amekubaliana na matokeo na ameshukuru kwa kuwa uchaguzi huo umemjenga,” inasema taarifa hiyo na kuongeza

 “Kilichotokea Arusha ni vurugu mitaani mbali na maeneo ya vituo vya kupigia kura, kwa kuwa vurugu hizo zilipelekea jinai kufanyika vyombo husika vinashughulikia. Hakuna chama chochote kilichojitokeza kusema na kuthibitisha kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki,” inasema taarifa hiyo iliyosainiwa na ofisa habari mwandamizi wa NEC, Christina Njovu

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuufahamisha umma kuwa Tanzania ni nchi huru na inaendesha chaguzi zake kwa mujibu wa Katiba yake na sheria za uchaguzi.”

NEC yajibu taarifa ya ubalozi wa Marekani kuhusu Uchaguzi Mdogo NEC yajibu taarifa ya ubalozi wa Marekani kuhusu Uchaguzi Mdogo Reviewed by KUSAGANEWS on August 15, 2018 Rating: 5

No comments: