Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka vijana wabadilike na
watafakari namna bora ya kuboresha maisha yao na wafanye kazi kwa bidii badala
ya kukaa vijiweni na kulalamika.
“Kama kuna changamoto
zinawakabili katika utekelezaji wa shughuli zao, basi tumieni njia sahihi
ikiwamo kuwasiliana na viongozi husika waliopo kwenye maeneo yao,” amesema
Amesema hayo jana jioni (Jumatano, Agosti 8, 2018) wakati
akizungumza na wakazi wa Kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye zahanati ya Kijiji cha Nandagala
Waziri mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mary Majaliwa katika
ziara yake ya kikazi wilayani Ruangwa, amesema vijana wanatakiwa kujitambua na
kuiunga mkono Serikali kwa kufanya kazi kwa bidii
Kadhalika, Waziri mkuu aliwataka vijana washirikiane kwa
pamoja katika kubuni shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato, jambo ambalo
litawakwamua kiuchumi na kuwawezesha kujitegemea
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewaeleza wananchi hao mikakati
mbalimbali inayofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo ya wilaya hiyo
ikiwamo upatikanaji wa huduma za afya pamoja na maji safi na salama
Pia, aliwataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali
yao, ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo kwa manufaa yao
na Taifa kwa ujumla
Waziri Majaliwa awataka vijana waache kulalamika
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment