Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, Suleiman Jafo ameiagiza Halmashauri ya Mji wa Geita kuanza kuwatoza
faini watu wanaotupa taka ovyo na kuharibu miundombinu ya barabara na madaraja
Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo Agosti,9,2018 wakati wa
ziara yake ya siku moja katika Halmashauri ya Mji wa Geita alipotembelea
ujenzi wa barabra ya lami na soko la kisasa miradi inayotekelezwa na fedha za
Serikali kuu na mapato ya ndani ya halmashauri
Amesema utunzaji wa mazingira ni jambo la msingi katika
kuleta maendeleo na kuzitaka halmashauri zote kuhakikisha madaraja yanayojengwa
yanatunzwa na kusimamiwa kutokana na tabia za wananchi kutupa taka ovyo
zinazosababisha madaraja kuziba
“Mkurugenzi hakikisheni mnaweka faini kwenye suala la
mazingira, Serikali inatumia fedha nyingi lakini wananchi wanatupa viroba na
takataka nyingine,”amesema Jafo
Katika ziara yake ya kutembelea soko la kisasa linalojengwa
mjini Geita aliutaka uongozi wa halmashauri kuhakikisha ujenzi unakamilika
haraka kutokana na muda aliopewa mkandarasi kumalizika
Waziri Jafo ataka wanaotupa taka watozwe faini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment