Muigizaji Steve Nyerere ambaye amekuwa mstari wa mbele
kuwaunganisha wasanii hasa katika kipindi cha misiba au matatizo yanayowatokea
wasanii wenzao, amepigwa benchi kwenye msiba wa Mzee Majuto
Hatua hiyo imekuja baada ya kuundwa kamati ya kushughulikia
msiba huo ambayo imeundwa na Chama cha waigizaji Mkoa wa Kinondoni (TDFAA)
pamoja na chama cha waigizaji Taifa
Kuondolewa kwa Steve ni kutokana na kutokuwa mwanachama
wa TDFAA, hivyo hawezi kuteuliwa katika kamati
Mara baada ya Mzee Majuto kufariki, wajumbe wa kamati
wakiongozwa na Simon Mwakifamba walifika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa
ajili ya taratibu za kuhifadhi mwili na wakatoa tamko kwamba taratibu zote za
kuaga zitafanyika Muhimbili na baadaye kusafirisha kwenda Donge, jijini Tanga
kwa maziko
Wakati hayo yakiendelea Steve Nyerere alifika Muhimbili saa
6.05 usiku, akija na utaratibu mwingine kuwa shughuli za kuaga zifanyike kwenye
viwanja vya Karimjee kwa kuwa Majuto ni mtu maarufu na tayari walishaanza kukaa
kikao na wasanii wenzake kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kuagiwa kwenye
viwanja hivyo
Hata hivyo, alipotoa wazo hilo, mmoja wa wanandugu
alijitambulisha kwa jina la Ashraf, alimwambia kuwa lazima wawasiliane na ndugu
wengine kwa hatua hiyo
Pamoja na wazo hilo kukubalika, Nyerere alibaki pembeni na
hata alipoulizwa zaidi kuhusu utaratibu alikataa kwa kuwa si mwanakamati wa
kamati ya maziko
“Mimi sihusiki na chochote kwani nimekuwa nikitukanwa kwamba
nakusanya fedha za rambirambi kisha nazitafuna,” anasema
Mzee Amri Athumani aliaga dunia jana majira ya saa
2:00 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa
amelazwa akitibiwa
Steve Nyerere apigwa benchi msiba wa Mzee Majuto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment