Mwili wa msanii wa vichekesho Amri Athumani ' King Majuto'
aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, utaagwa leo Agosti 9,
2018 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
Rais wa shirikisho la filamu Tanzania , Simon Mwakifamba
amesema, Mzee Majuto ataagwa kuanzia saa 8.00 mchana katika viwanja hivyo na
saa 10.00 jioni atasafirishwa kwenda nyumbani kwake Tanga kwa mazishi
“Taarifa ambayo tumewasiliana na familia ni kwamba, Mzee
Majuto ndugu jamaa na marafiki watatoa heshima za mwisho na baada ya hapo mwili
utaelpelekwa nyumbani kwake Tanga kwa ajili ya mazishi,” amesema Simon
Mwakifamba
Kwa upande mtoto wa Mzee Majuto, Ashrafu amesema,ratiba
kamili ya mwili wa Mzee Majuto ni kwamba asubuhi mwili utaandaliwa katika
Hospitali ya Muhimbili na shughuli zote ndogo ndogo zitafanyika hapo,
baada ya hapo mwili utapelekwa Karimjee kwa ajili ya kuagwa saa nane
mchana," anasema
Akielezea saa za mwisho za Mzee Majuto Ashrafu anasema:
“Hali yake ilibadilika majira ya saa 9.00 alasiri jana hivyo kuhamishwa kutoka
jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake
ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio.
Ilipofika saa 2 usiku alifariki,''
Amri Athuman’ King Majuto’ alizaliwa 1948 jijini Tanga na
kusoma shule Msambweni, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka tisa
akiigiza katika majukwaa
Mzee Majuto ambaye alikuwa mtunzi, muigizaji, mwandishi wa
mswada na pia ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na
kuuza akiwa na Tanzania Film Company (TFC
Mzee Majuto kuagwa viwanja vya Karimjee leo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 08, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment