Jeshi la polisi , wilayani Tarime
mkoani Mara, linawashikilia Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko, pamoja na
mwandishi wa habari, mara baada ya kuamuru wanachama wa chama cha demokrasia na
maendeleo (CHADEMA), kusitisha kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea nchini.
Mkutano ambao pia ulihudhuriwa na
kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, pamoja na mbunge wa Viti
Maalumu (Chadema) mkoa wa Geita Upendo Peneza mara baada ya zuio hilo viongozi
hao waliandika katika kurasa zao za mitandao ya kijamii huku lawama zote
wakizielekeza kwa Jeshi la Polisi.
“Jeshi la Polisi linaamuru
tuache mkutano wa hadhara hapa Tarime. Mkutano wa kampeni ambao upo kwenye
ratiba ya Tume ya Uchaguzi. Msimamizi wa uchaguzi kaamuru mikutano yote ya kata
ya Turwa isimamishwe”, ameandika Zitto
Kusaganews tumemtafuta Kamanda wa Polisi
Wilayani Tarime Rorya, Henrry Mwaibambe amesema kuwa wanamshikilia Mbunge huyo
kwakile alichodai kuwa alikuwa akihamasisha maandamano ya wafuasi wa Chadema.
“Msimamizi wa kituo cha
uchaguzi ametuandikia barua akitutaarifu kuzuia kwa mkutano wa hadhara kwa
wanachama wa Chadema kwakuwa wamesimamishwa kufanya kampeni kwa muda wa siku
nne baada ya kukiuka maadili ya uchaguzi”, amesema Kamanda Mwaibambe.
Sababu za kukamatwa Mbunge wa Tarime mjini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 09, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment