Waziri atumia baiskeli kwenda hospitali kujifungua


Katika hali isiyo ya kawaida waziri anayehusika na Masuala ya Wanawake nchini New Zealand ametumia usafiri wa baiskeli kuelekea hospitali kwa ajili ya kujifungua

Waziri huyo Julie Genter anayetoka chama cha Kijani alisema kwamba aliamua kutumia usafiri huo kwa sababu gari lake halina nafasi ya kutosha

Kiongozi huyo alipiga picha na mume wake wakielekea hospitali kwa kutumia usafiri huo wa baikeli na kuiweka katika akaunti yake ya Instagram

Kuanzia mwezi wa sita mwaka huu Mbunge, Jacinda Ardern na Genter walikua wakihudhuria kliniki pamoja katika hospitali moja iliyopo mjini Auckland

Genter 38, aliyejifungua mtoto wa kwanza aliandika katika mtandao wake wa Instagram, ''mtuombee, mimi na mwenzangu tumepanda kwenye baiskeli kwa sababu hakukua na nafasi’’

Mbunge wa kwanza kupata mtoto akitumikia bunge la New Zealand, ilikua mwaka 1970, huku mwingine akinyonyesha kwa mara ya kwanza katika eneo la kazi mwaka 1983

Waziri atumia baiskeli kwenda hospitali kujifungua Waziri atumia baiskeli kwenda hospitali kujifungua Reviewed by KUSAGANEWS on August 20, 2018 Rating: 5

No comments: