Serikali imatoa ajira kwa watumishi 2,160 katika shule za
sekondari nchini ambapo kati yao waalimu 1900 ni wa masomo ya sayansi na
hisabati
Akizungumza leo jumatatu Agosti 20,2018 Waziri wa nchi ofisi
ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amesema kati ya watumishi hao walioajiriwa 100
ni waalimu wa lugha na 160 ni fundi sanifu maabara
Amesema watumishi hao wanatakiwa kuripoti katika ofisi za
wakurugenzi wa halmashauri zilipo shule walizopangiwa kuanzia Agosti 23,2018
hadi Septemba 5,2018
“Watumishi hao wanatakiwa kuripoti kwa muda huo wakiwa na
vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne na kidato cha sita, vyeti halisi
vya kitaalam vya mafunzo ya ualimu vya ngazi husika pamoja na cheti cha
kuzaliwa, na hatimaye kwenye shule walizopangiwa” amesema Jafo
Hata hivyo, Jafo amewataka waajiriwa hao kuripoti kwenye
vituo vyao vya kazi na si makao makuu ya halmashauri ili kuomba kuhamishiwa
vituo vya kazi
“Mwajiri yeyote atakayechukua posho ya kujikimu kisha
asiripoti kwenye kito chake cha kazi serikali itamchukulia hatua za kinidhamu,”
amesema Jafo
Jafo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakurugenzi wa
halmashauri zenye vituo vya kazi walizopangiwa watumishi hao kuwapokea na kwa
kufuata taratibu zote na kanuni za utumishi
Serikali yaajiri walimu 2160
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 20, 2018
Rating:
![Serikali yaajiri walimu 2160](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhdPJ60-OWTHTdZqAQb9Dq0O-w29s5QKeNNC0vfNUScxwLpwfY_CdpHh_n6Bv5pP81WA4N3KQ5MWcKo6_D5dqhE3qTkIwZ2ocALwmSoTrgvZt518xht4sRfC4i_ay_vWMfaBxa_L4zp0AI/s72-c/4.jpg)
No comments:
Post a Comment