Babati. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elexander Mnyeti juzi,
amezindua ligi ya Chemchem ,inayoshirikisha timu 20, yenye lengo la kupiga vita
ujangili ambayo itagharimu zaidi ya sh 35 milioni.
Akizungumza katika uzinduzi huo katika viwanja vya
mdori, wilayani Babati, Mnyeti ambaye aliwakilishwa na Kamanda wa polisi mkoa
wa Manyara, Augustine Senga alitaka timu zitakazoshiriki kucheza kwa nidhamu
ili kufikia malengo ya ligi hiyo.
Mnyeti alisema,ligi hiyo pia inapaswa kutumika katika
kuibua vipaji kwa wachezaji chipukizi ili kuweza kusajiliwa katika timu za ligi
kuu.
"najua hapa kuna vipaji hivyo michezo hii ni fursa
ya kujulikana zaidi na hivyo kuwa sehemu ya kutoa ajira kwa vijana na kujenga afya"alisema
Katibu wa mashindano hayo,John Bura alisema jumla ya
timu 20 za soka zinatarajia kushiriki michuano hiyo na kutakuwa na zawadi kwa
mshindi wa kwanza hadi wa nne.
"pia kutakuwa na ligi ya wanawake ambayo
itashirikisha timu tatu na washindi watapewa zawadi"alisema
Alisema katika michuano hiyo, mchezaji bora,mfungaji
bora na timu yenye nidhamu, watapata zawadi na hivyo, akawataka kucheza soka la
kuvutia
Awali Meneja wa Chemchem ambao ni wadhamini wa ligi
hiyo, Kanali mstaafu,Leonard Werema alisema, taasisi hiyo, inayofanya shughuli za Utalii katika eneo
hilo la hifadhi ya jamii ya
Wanyamapori(WMA) ya
burunge, inataka ligi hiyo, kusaidia kutoa elimu ya kupiga vita ujangili
na uhifadhi.
Werema alisema Chemchem imegharamia zaidi ya sh 35
milioni katika michuano hiyo, ikiwepo kuandaa uwanja na majengo kadhaa,zawadi,
imetoa vifaa vya michezo kwa timu zote 23 na gharama nyingi za waamuzi na
waratibu wa michuano hiyo chama cha soka wilaya ya Babati.
Katika mchezo wa ufunguzi, mabingwa watetezi, Mdori FC
walipata ushindi wa magori 3-2 dhidi ya timu ya City Boys katika mchezo mkali
uliochezwa kiwanja cha mdori.
RC Manyara azindua ligi cha Chemchem Babati iliyogharimu sh 35 milion.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment