Jeshi la Polisi mkoani Iringa
linawashikilia watu wawili waliokuwa wakiwasafirisha wanafunzi watano wa shule
ya sekondari ya Mlafu kwenda Dar es Salaam kufanya kazi za nyumbani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,
Kamishna Msaidizi (ACP), Juma Bwire, alisema tukio lilitokea Julai
31, mwaka huu, katika mji mdogo wa Ilula, Kilolo mkoani Iringa.
Bwire alisema watuhumiwa hao
walikuwa wakihangaika kuwasafirisha kwa ajili ya kuwatumikisha kazi za ndani,
baada ya wanafunzi hao kutoweka kwa wazazi wao tangu Julai 29 mwaka huu na
walisafirishwa kwa bodaboda kutoka Mlafu hadi Ilula.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni
Tulizo Mtega (19) na Rosemary Msasalage (18) wote wakazi wa Ilula na kwamba
mbinu iliyotumika kuwarubuni wanafunzi hao ni kuwa wamepata kazi mbalimbali za
kuuza maduka Morogoro na Dar es Salaam.
Wawili Watiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kuwatorosha Wanafunzi na Kuwapeka Dar Wakafanye Kazi za Ndani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment