Msanii wa filamu, Rehema Abdallah amesema marehemu Amri
Athuman maarufu kama Mzee Majuto licha ya kuwa alikuwa amelazwa Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH), alikubali kurekodi sehemu ya filamu akiwa katika
hospitali hiyo.
Rehema ambaye ameigiza na Mzee Majuto tangu mwaka 1978
akicheza mara nyingi kama mkewe, amesema siku chache kabla Majuto hajaanza
kumwa alimshauri aanzishe kikundi cha maaigizo Mombasa kutokana na kuwa na
mashabiki wengi huko na kuahidi angemsaidia
Amebainisha kuwa katika mchakato huo alikuwa akimpelekea
baadhi ya nyaraka na kuzisaini akiwa MNH na pia alimuahidi atacheza baadhi ya
vipande hata kama atakuwa bado amelazwa
“Nasikitika hilo la kuigiza na kukamilisha mchakato wa
kikundi hicho halijakamilika mzee wetu katutoka, huenda ingekuwa ni kumbukumbu
nzuri kwa Watanzania,” amesema
“Kwani mtu kukubali kucheza hadi akiwa kalazwa hospitali si
jambo dogo, ingeacha funzo kwa wasanii namna gani tunatakiwa tuipende kazi yetu
bila kujali upo katika hali gani.”
Kuhusu mahali walipokuwa wamefikia katika uanzishwaji wa
kundi hilo, Rehema amesema tayari walishapata wasanii 70, walikuwa katika
hatua za mwisho za kuanza kufanya kazi
Hata hivyo, amesema hajui kama kundi hilo litaweza kuendelea
kwa maelezo kuwa mchango wa Mzee Majuto bado ulikuwa ukihitajika kwa kiasi
kikubwa katika kufanikisha uanzishwaji wake
“Mzee Majuto ndiye alikuwa ananishika mkono na kunielekeza
wapi pa kwenda katika kukamilisha masuala mbalimbali yaliyohitajika kwa ajili
ya kikundi sasa leo nani atanisaidia kufanya hivyo, yaani sioni tena mwanga
mbele wa kulifanikisha hili, namuachia Mungu ndiye aamue,”amesema Rehema
Mzee Majuto alifariki Agosti 8 mwaka huu akiwa anapatiwa
matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili na anatarajiwa kuzikwa leo
kijijini kwake Kiruku Tanga
Majuto alikuwa tayari kuigiza akiwa Hospitalini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment