Katibu Mkuu Chadema Dk Vicent Mashinji, mwenyekiti wa chama
hicho Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa na katibu wake, Emmanuel Masonga
wamewasili katika mahakama ya wilaya ya Mbozi, Songwe kusikiliza hukumu ya
Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga
Haonga na wenzake, Wilfredy Mwalusamba (katibu wake) na
Mashaka Mwampashi wanakabiliwa na makosa matatu ya kufanya fujo na kuvuruga
mkutano wa uchaguzi wa baraza la mji mdogo wa Mlowo, kosa la pili na tatu
ni kuwazuia askari kutekeleza majukumu yao
Wanadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 28, 2017, na leo Ijumaa
Agosti 10, 2018 mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo
Mbali na viongozi hao, pia wananchi na wafuasi wa Chadema
wameanza kumiminika katika mahakama hiyo huku ulinzi ukizidi kuimarishwa
kutokana na askari kutanda kila kona wakiwa na silaha za moto
CHADEMA wajazana mahakamani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment