Hofu imetanda miongoni mwa wakazi wa vijiji vya Misasi,
Isakamawe na Mabuki wilayani Misungwi mkoani Mwanza baada ya maiti za wanawake
wanne kuonekana huku zikiwa hazina baadhi ya viungo.
Miili hiyo imeokotwa
maeneo tofauti ikiwa na alama zinazoonyesha walinyongwa kabla ya kufariki
John Makoye mkazi wa Isakamawe aliyeshuhudia maiti ya
marehemu hao ametaja baadhi ya viungo vilivyonyofolewa kuwa ni ulimi, matiti na
sehemu ya siri
Akizungumza leo Ijumaa Agosti 3, 2018 kamanda wa polisi mkoa
wa Mwanza, Ahmed Msangi amewataja waliouawa kuwa ni Angelina Lumala (45)
mkazi wa kijiji cha Isakamawe, Kundi Laurent (35) na Mariamu Manila (30) wote
wakazi wa kijiji cha Misasi na mmoja aliyetambulika kwa jina la Ngole (43)
mkazi wa Kitongoji cha Bujingwa kijiji cha Mabuki
Amesema polisi tayari inawashikilia kwa mahojiano watu
watatu ambao hakuwa tayari kuwataja majina waliokutwa kwenye mapori ambako
miili hiyo ilikutwa
Akizungumza na familia za marehemu baada ya kuzitembelea,
Kamanda Msangi amewaomba wananchi wenye taarifa zitakazosaidia kuwanasa wauaji
kujitokeza kusaidiana na polisi
"Si tukio la kawaida watu wanne kutoka maeneo na vijiji
tofauti kuuawa katika mazingira yanayofanana. Kuna dalili za mauaji haya
kuhusishwa na imani za kishirikina zinazotokana na ramli chonganishi.
Tutawasaka na kuwatia mbaroni wote waliohusika na matukio haya,” amesema
Kamanda Msangi
Kaimu mkuu wa wilaya ya Misungwi, Marco Peter amewataka
akina mama wanaokwenda porini kukata kuni kuchukua tahadhari na kuwa katika
makundi na ikiwezekana waongozane na waume zao
“Viongozi wa vitongoji na vijiji nao wanapaswa kuimarisha
vikundi vya ulinzi wa jadi maarufu kama Sungusungu katika maeneo yao kwa ajili
ya ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao,” amesema
Wanawake wanne wauawa, wanyofolewa viungo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment