Unaweza kusema mkoa wa Dodoma kuongoza kwa mapato kati ya
majiji sita yaliyopo nchini kumemtikisa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Paul
Makonda
Leo Ijumaa Agosti 3, 2018 Makonda amemtaka katibu tawala wa
mkoa huo, Abubakar Kunenge kukutana na wakurugenzi wa halmashauri zote za jiji
hilo kupitia taarifa za mapato ili kubaini sababu za Dar es Salaam kupitwa na
Dodoma katika ukusanyaji wa mapato
Ametoa kauli hiyo katika hafla ya kuwakaribisha wakuu wa
wilaya wapya na kuwaaga waliohamishwa vituo vya kazi
Makonda amesema lazima wakurugenzi wa Dar es Salaam waongeze
vyanzo vya mapato, kusimamia taarifa za mapato katika halmashauri zao
"Haiingii akilini tumezidiwa na Dodoma kwenye ukusanyaji
wa mapato, tutafanya kila namna kurejea katika nafasi yetu," amesema
Makonda akimueleza Kunenge aliyechukua nafasi ya Theresia Mbando aliyehamishiwa
mkoa wa Pwani
Mapato madogo Dar yamuumiza kichwa Makonda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment