MWANAMKE mkazi Njage
wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro, ameuawa kwa kukatwa kwa shoka kichwani na
mumewe kwa kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi
Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, mwanaume huyo baada ya
kumuua mkewe kwa kumkata kwa shoka kichwani, alikimbilia porini na kujinyonga
kwenye mti kwa kutumia kamba
Kamanda Mutafungwa alisema inadaiwa kuwa mwanaume huyo
aliamua kufanya kitendo hicho baada ya kuona mkewe amempuuza alipomwambia
kuwaondoa watoto wake wa kike aliowazaa nje ya ndoa
Kamanda alifafanua kuwa alitaka waende kwa waliomzalisha
watoto hao kwa madai kuwa wanawanyima nafasi wakiwa hapo
Alisema miili ya marehemu hao imeshakabidhiwa kwa ndugu zao
kwa ajili ya kuendelea na shughuli za mazishi
Katika tukio lingine, Leo Charles Mashaka (61), mkazi wa
Kitongoji cha Igagafu wilayani Kilosa, ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye butu
kichwani na usoni na mtoto wake wa kumzaa, Emmanuel Leo Charles, sababu
ikitajwa ni kudai urithi
Kamanda Mutafungwa alisema tukio hilo lilitokea Julai 30,
alfajiri katika Kata ya Lumuma Tarafa ya Idete ambapo Mashaka alimpigwa na kitu
chenye butu kichwani na usoni upande wa kulia na kumsababishia jeraha na
michubuko mgongoni
Alisema tukio hilo lilisababishwa na mgogoro katika familia
kuhusu urithi
Kamanda huyo alisema mtuhumiwa alikamatwa na atafikishwa
mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika
aua mke kwa shoka ajinyongakwa kamba kisa wivu wa-mapenzi'
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment